in

Indo Solutions Yashutumiwa Baada Ya Kukiuka Mkataba Wa Korosho Na Nchi Ya Tanzania

indo solutions, tanzania
ACT Wazalendo leader Zitto Kabwe [Photo/Courtesy]

Kampuni ndogo kutoka Kenya ambayo ilijishindia kandarasi ya kununua korosho kutoka nchi jirani ya Tanzania bado haijafanya malipo yoyote mpaka sasa, hii ni kulingana na Kiongozi wa chama cha Wazalendo Zitto Kabwe Ruyagwa.

Kabwe Ruyagwa anadai kuwa Indo Power Solutions Ltd ambayo ilitarajiwa kulipa dola milioni mia moja na themanini nuka mbili ($180.2/TZS 400B)haijawasilisha pesa zozote kwa mujibu wa mkataba wa pamoja na LC Magumashi.

Akizungumza kupitia mtandao wa jamii wa Twitter siku ya Jumanne, Ruyagwa aidha alisema kuwa korosho bado hazijaweza kusafirishwa baada ya mabenki ambayo yalitarajiwa kufadhili shughuli hiyo kugoma.

“Ile Kampuni ‘hewa’ kutoka Kenya iliyoingia mkataba wa kununua Korosho tani 100K kwa US$180m (TZS 400b) mpaka sasa haijalipa pesa kwa mujibu wa mkataba pamoja na LC magumashi, ” Ruyagwa alisema.

“Korosho hazijabebwa na mabenki ya ndani yaliyofuatwa kutoa pesa yamegoma. Serikali ya CCM

Aliilaumu Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoongozwa na raisi John pombe Magufuli kwa kukosa kutoa mwongozo bora.

Kampuni ya Indo Power Solutions ikiwakilishwa na mkurugenzi mtendaji  Brian Mutembei  iliingia katika mkataba wa kununua korosho kutoka kwa wakulima wa nchi ya Tanzania mnamo Januari 30 mwaka huu. Hii ni baada ya kuzipiku kampuni zingine nane zilizokuwa zimeonyesha nia katika biashara ya korosho.

Licha ya kampuni hiyo kutotambulika hau kuwa na uzoefu wa kununua au kuuza korosho ilipewa kandarasi hiyo.

Read: Rais Magufuli Atoa Shilingi Milioni 200 Kufadhili Kituo Cha Redio Cha Magic FM, Kinachomilikiwa Na CCM

Mkurugenzi wa bodi ya nafaka nchini Tanzania Hussein Mansour aliidhinisha mkutaba huo katika makao makuu ya Jumuia ya Afrika mashariki mjini Arusha.

Vile vile, waziri wa sheria Palamagamba Kabudi, waziri wa biashara Joseph Kakunda na gavana mkuu wa benki kuu ya Tanzania Florens Luoga ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla iyo.

Email your news TIPS to news@kahawatungu.com or WhatsApp +254708677607. You can also find us on Telegram through www.t.me/kahawatungu

Written by Wycliffe Nyamasege

Email news@kahawatungu.com

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

robert chesang

Shot Lawyer, Robert Chesang’s Marriage Was Allegedly In Shambles

EACC Raids Samburu Governor Moses Lenolkulala’s Homes Over Ksh2 Billion Scandal