in ,

IEBC Kununua Masanduku Mengine Mapya Kwa Ajili ya Marudio ya Uchaguzi

chiloba
IEBC Chairperson, Ezra Chiloba
nasa
IEBC CEO Ezra Chiloba

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imetangaza kwamba itanunua masunduku mengine ya kupiga kura kwenye marudio ya uchaguzi wa kiti cha urais unaotarajiwa Oktoba 17, 2017.

Baada ya majaji wa mahakama ya upeo Jumatano kutoa maelezo kwa undani kufuatia kubatilishwa kwa ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa Jubilee wa Agosti 8, wakili wa IEBC Paul Muite aliwasilisha pendekezo kwa Jaji Mkuu David Maraga kura zilizopigwa zitolewe ili masanduku hayo yatumike.

“Tayari mmetoa uamuzi ambao kwa vyovyote vile hautabadilishwa ila kurejea debeni. Uchaguzi uliopita taifa limegharamika kiasi kikubwa cha pesa, ninaomba kwa heshima zako Jaji Mkuu kura zilizohifadhiwa kwa masanduku zilitolewe ili yatumike kwenye shughuli ijayo,” akaomba Bw Muite kwenye mahakama hiyo jijini Nairobi.

Akaongeza: “Ikiwezekana kura hizo zihifadhiwe katika mahakama hii kwa sababu za kiusalama.”

Hata hivyo swala hilo lilipingwa vikali na wakili wa National Super Alliance (Nasa) James Orengo ambaye alipata agizo la mahakama kuhifadhi masanduku hayo kwa miaka mitatu zaidi. “Mheshimiwa Jaji masanduku hayo hayafai kufunguliwa kwa mujibu wa sheria. Yanafaa yasalie yamefungwa kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kwa sababu za kuzirejelea usoni endapo kutakuwa na msukumo,” akaeleza Orengo, ambaye pia ni Seneta wa Siaya.

Kauli ya Bw Orengo iliungwa mkono kwa dhati na wakili aliyewakilisha Rais Kenyatta na Jubilee Party (JP) Fred Ngatia.

“Ninaomba ombi la Wakili Muite lifutiliwe mbali. Kura hizo huenda zikatufaa baadaye ikiwamo kuthibitisha aliyeibuka mshindi,” akaeleza Bw Ngatia.

Hata hivyo Muite alibadilisha ombi lake baada ya kufahamishwa kwamba tume ya IEBC itanunua masanduku mengine. “Nimefahamishwa kuwa IEBC itanunua masanduku mengine. Naomba mahakama itupilie mbali hilo ombi langu,” akasema na kusababisha watu kuangua kicheko mahakamani.

Muungano wa Nasa ulipinga ushindi wa Rais Kenyatta mahakamani ambapo Jaji Maraga aliagiza IEBC iandae uchaguzi mpya wa urais kwa siku 60.

Mrengo wa Jubilee umekashifu uamuzi wa mahakama hiyo ukishitumu Maraga kushirikiana na Nasa kuwapokonya ushindi.

Bw Raila Odinga ndiye kinara mkuu wa Nasa.

Do you have a story you want told? Do you know of a sensitive story you would like us to get our hands on? Email your news TIPS to news@kahawatungu.com

Written by Kahawa Tungu

Email: news@kahawatungu.com

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Exclusive: Raila Opens Up About Elections, DP Ruto, Says He Suffers From Amnesia

Is Huddah Monroe ‘Team Zari’ Or ‘Team Diamond’?